Hili ni Moja ya jengo katika
Zahanati ya Kabasa
Imeelezwa
kuwa Zahanati ya kijiji cha Kabasa kata
ya kabasa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara haina muuguzi anayeishi
katika eneo la kazi wote wanaishi mjini Bunda licha ya kuwepo nyumba za kuishi
wauguzi katika zahanati hiyo.
Hayo
yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa nyakati tofauti wakati
wakizungumza na radio Mazingira fm kijijini hapo.
BI NYAMJINJA pamoja na BI MILKA Wamesema kutokuwepo karibu wauguzi
katika eneo la kazi wanapata wakati mugumu wanapokuwa na mgonjwa hasa nyakati
za usiku hali ambayo inasababisha kutumia gharama kubwa ya usafiri kumfikisha mgonjwa katika
Hospital ya wilaya kwani kunaumbali kutoka kijijini hapo.
Wamesema
kuwa wanashangaa kuona wauguzi wote wa zahanati hiyo kuishi mjini wakati nyumba zipo za kuishi wao katika zahanati
hiyo.
Aidha wamesema
kuwa ikifika saa tisa alasiri wauguzi huondoka katika eneo la kazi na kuelekea
mjini wanakoishi hivyo kuanzia muda huo hakuna mtu yeyote anayepata huduma
katika zahanati hiyo.
Radio
mazingira amezungumza na mmoja ya wauguzi kwa masharti ya kutotajwa jina
ameseme ni kweli hawaishi hapo kutokana na nyumba hizo kuonekana zinahitilafu hivyo
zikilikebishwa wataishi hapo na kwamba suala lakufunga zahanati hiyo na kutoka
saa tisa ni kwa mujibu wa sheria sio kwamba wamejitungia wenyewe.
Hata hivyo tulipomtafuta
mtendaji wa kata ya Kabasa ELISHA HENRY
amesema kuwa kitendo cha wauguzi kusema kuwa nyumba ni mbovu wakati hata
hawaishi hapo si la msingi hivyo wao waanze kuishi kama marekebisho yatafanyika
bila shida yeyote kwani lipo ndani ya uwezo wao.
Elisha amesema wanahofia kutumia gharama
bure kufanya ukarabati kabla ya kuona wauguzi wakiishi hapo hivyo wao wauguzi
waanze kuishi ukarabati utafanika bila shida.
Moja
ya nyumba inayotajwa kuwa ndo ya kuishi wauguzi
Elisha Henry mtendaji
wa kata ya Kabasa
No comments:
Post a Comment