Wakazi wa mtaa wa Bigutu katika halmashauri ya mji wa
Bunda mkoani Mara wameipa jina la mbunge wa Bunda mjini barabara yenye urefu wa
kilomita moja pointi tisa baada ya jitihada za mbunge huyo za kuwafikishia
huduma ya barabara ambayo wameikosa kwa muda mrefu.
Wakizungumza katika mkutano
uliofanyika siku ya ijumaa ikiwa ni sehemu ya ziara ya mbunge huyo ya kukagua
utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia mfuko wa jimbo wananchi hao wamesema
kuwa wanampongeza mbunge huyo kwa kuwafikishia barabara ambayo itachochea maendeleo
mtaani hapo.
Wananchi hao wamesema kuwa wameamua
kuipa jina la ester bulaya barabara hiyo
ikiwa ni kumbumbu na jitihada za mbunge huyo za kuwaletea maendeleo katika eneo
lao kwani wameonekana kuwa wamesahaulika kwa mda mrefu.
Naye mbunge wa jimbo la Bunda mjini
Ester buyala amesema kuwa uwepo wa barabara hiyo utawasaidia wakazi wa eneo hilo kutatua
changamoto ndogondogo zinazowakabiri.
No comments:
Post a Comment