Waendesha bodaboda katika
Wilaya ya Bunda Mkoani Mara wamepewa miezi miwili kukata leseni ya usafirishaji abiria kabla
serikali kuanza kuwachukulia hatua wale ambao watakuwa hawajatekeleza maelekezo
hayo.
Wito huo umetolewa na
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa bunda Janeth Mayanja katika kikao
kilichowakutanisha pamoja waendesha bodaboda, Jeshi la Polisi, ofisi ya mkuu wa
wilaya pamoja na ofisi ya Sumatra mkoa Mara.
Aidha katika kikao
hicho,Afisa Mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti Usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA
Mkoani Mara Halima Lutavi amewaeleza madereva hao kuwa leseni hizo
wanapaswa kulipa kwa mujibu wa sheria lakini mjini bunda zoezi hilo limechelewa
kuanza kutokana na kwamba imeanzishwa hivi karibuni, ambapo amesema kwamba
leseni hizo zitatolewa na afisa biashara wa halmashauri ya mji wa bunda.
Hata hivyo Mkuu wa
wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili amesema lengo la serikali ni kutambua
waendesha pikipiki maaarufu kama bodaboda na kuwawekea mazingira rafiki ili
kunufaika na kazi zao.
Kwa upande wa madereva
bodaboda wamesema kuwa wamepokea maelekezo ya serikali na wameahidi kuyafanyia
kazi.
No comments:
Post a Comment