Dc Bunda awaonya wanawake kutofurahia wanapoona wenzao wanapigwa na waume zao. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday, 9 March 2018

Dc Bunda awaonya wanawake kutofurahia wanapoona wenzao wanapigwa na waume zao.



Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl, Lydia Bupilipiliamewataka wanawake kuwa wamoja katika kukemea vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa na waume wao,hasa vipigo.

Amesema kuwa wanawake wanaoshangilia na kufurahia  wanapoona wanawake wenzaowakipigwa wasidhani kwa upande wao wako salama kwakuwa baada ya mwingine kipigo hicho kitahamia kwao.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Marambeka, kata ya Ketare wilayani hapo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Aidha ameitaka jamii kuondokana imani potofu zilizopitwa na wakati kama kukataza watoto wa kiume kufanya shughuli za nyumbani na kuwaachia watoto wa kike  wenyewe, kwani kufanya hivyo ni kuendeleza unyanyasaji wa kijinsia na kuwakosesha watoto wa kike fursa za maendeleo.

Pamoja na hayo lakini pia  Mkuu huyo wa wilaya kupitia maadhimisho hayo amepokea vifaa vya maabara vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 10 milioni katika shule ya sekondari espiranto,
kutoka kwa marafiki wa Diwani wa kata ya Ketare Simba Mramba Nyamkinda.

Wafadhili hao wanaofanya kazi na shirika lisilo la kiserikali la Mazingira Faundeshen wamesema kuwa watashirikiana na serikali ya tanzania kusaidia wananchi na hasa wanaoishi vijijini ili kuwaletea maendeleo na kupata wataalam watakaosaidia katika taasisi mbalimbali.

Hata hivyo Bupilipili amewashukuru wafadhili hao kwa kuona umuhimu wa kusaidi shule ya sekondari espiranto vifaa hivyo ikizingatiwa kuwa shule nyingi nchini bado wanakabiliwa na mapungufu ya vifaa hivyo muhimu vya maabara.

No comments:

Post a Comment