Imeelezwa kuwa Serikali imetangaza utaratibu mpya utakaotumiwa
na wakulima wa kilimo cha pamba kuuza zao hilo
ifikapo msimu wa pamba mapema mwezi mei mwaka huu.
Utaratibu huo umetolewa na waziri wa kilimo
Dr.charles Tizeba alipokuwa kwenye ziara yake wilayani Bunda mkoani
Mara ya kuangalia maandalizi ya masoko katika
msimu wa kuuza kahawa na pamba
unaotarajiwa kuanza mapema mwezi mei.
Dr.Charles amewasisitizia
wakulima wa zao hilo kufata utaratibu
huo wakujiunga katika vyama vya ushirika
vilivyopo katika maeneo yao kwani atakaye
kiuka hataweza kuuza pamba yake mahali popote na kuongeza kuwa utaratibu huo
utatumika nchi nzima.
Akitangaza
kuanza kwa msimu wa zao la pamba waziri
Tizeba amesema kuwa msimu utafunguliwa rasmi mei mosi ambapo amewambia wakulima wasiwe na wasiwasi kuhusu bei ambayo
itatangazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment