Kikundi cha
Maisha Kinamama kilichopo katika
halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara kimepewa mkopo wa hundi ya shilingi
milioni nne ikiwa ni njia ya kumkomboa mwanamke kiuchumi.
Akikabidhi
hundi mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi
Jannet Mayanja kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyo fanyika kwenye
viwanja vya Guta amewataka wanakikundi hao kutumia pesa hizo kwa malengo ili
waweze kuondokana na hali tegemezi.
Pamoja na
hayo Bi Mayanja amewataka wananchi wote
kuungana na kushirikiana kwa pamoja katika kuzuia na kutatua vitendo vya kikatili vinavyofanywa kwa wanawake pamoja
na kuleta maendeleo kwa wanawake ili
waweze kujikwamua kiuchumi huku
akiwaomba wanaume wote kuwaunga mkono wanawake kuhakikisha haki ya mwanamke
inapatikana.
Akisoma
risala kwa mgeni rasmi afisa maendeleo
Stella Kazinja ametaja changamoto zinazokwamisha kumuwezesha mwanamke
kiuchumi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kuwa ni
uelewa mdogo katika jamii kuhusu usawa wa kijinsia ambapo swala hili limefanya mwanamke
kutothaminiwa mchango wake katika mafanikio mengi ambayo yanapatika katika
maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment