Tume ya Haki za Binadamu Yafungukia Matukio ya Uchaguzi
Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetoa taarifa kwa umma
kuhusu tathimini juu ya matukio yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi
mdogo wa marudio uliofanyika katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es
Salaam, na Siha mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi msaidizi wa kituo hicho,
Anna Henga, amesema katika kipindi cha kampeni waliona matumizi ya
watoto katika kampeni, na kushuhudia video ya mtoto akinengua na
kutumbuiza jukwaani katika kampeni za chama cha mapinduzi (CCM), kitu
ambacho ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki za binadamu hususani kwa
watoto.
Pia kituo hicho kilishuhudia matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi
ya vyama, kitendo ambacho kilifanywa na CCM katika jimbo la Siha kumnadi
mgombea wao Dkt Mollel.
Aidha kituo hicho kimebainisha kuwa kiliona matumizi ya nguvu katika
kipindi cha kampeni yaliyopelekea raia kuumizwa na kusababisha kifo cha
mwanafunzi wa (NIT), Akwilina Akwilini, Februari 16, kilichosababishwa
na jeshi la polisi walipokuwa wakidhibiti maaandamano ya Chadema, na
kuwashikilia raia 40.
Na Katika siku ya kupiga kura, kituo hicho kimeshuhudia mwitikio mdogo
wa wapiga kura, unyanyasaji wa mawakala wa vyama vya siasa kwa kutopewa
kwa wakati viapo.
Thursday, 1 March 2018
BREAKING NEWS: Tume ya Haki za Binadamu Yafungukia Matukio ya Uchaguzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment