Mbunge wa Serengeti,mkoani Mara
Marwa Ryoba Chacha (CHADEMA) ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha polisi
kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge wa Tarime Vijijini CHADEMA, Mhe. John Heche kwa
kile kinachodaiwa kuhofia maandamano yanayoratibiwa na Mange Kimambi.
Marwa Ryoba amesema kuwa polisi
wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu wa CCM wakiendelea kufanya
maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali watu wa upinzani wakizuiliwa.
"Haki huinua taifa; bali dhambi
ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh.
John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange
Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu"
,alisema Mbunge Marwa Ryoba
Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini
kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na
jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu
ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne.
"Ni kweli polisi walitaka
kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka
kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya
tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi
wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.
No comments:
Post a Comment