KILA kukicha
wanatokea manabii wanaokuja na staili mbalimbali za mahubiri na miujiza ya kila
aina, wakati Nabii Tito ambaye alikuwa akihubiri mitaani kwamba kuzini na
kulewa siyo dhambi, akisota Hospitali ya Mirembe mkoni Dodoma, baada ya
kuonekana kwamba ana matatizo ya akili, mwingine aliyetambulika kwa jina la
Daniel Daniel Shilla (22), ameibuka na kutikisa Jiji la Dar. Nabii huyo mtoto
ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kugawa pesa kwa waumini
wanaosali kanisani kwake, anaongoza kanisa linalojulikana kwa jina la Bethel
International Ministry Of Tanzania, lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba na
Kigamboni kwa jijini Dar na matawi mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Zanzibar,
Kigoma, Morogoro na mengineyo.
Baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito za kuwa na
utajiri mkubwa usiokuwa na vielelezo, kuusishwa na Freemasons na masuala ya
utapeli kwa wanaohitaji huduma zake za maombezi, Ijumaa Wikienda liliamua
kumsaka Nabii Shilla na kukuletea stori kamili.
No comments:
Post a Comment