Ndani ya Halmashauri ya mji wa Bunda huenda ikafungwa Shule nyingine tena kwa tatizo la choo. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday, 6 March 2018

Ndani ya Halmashauri ya mji wa Bunda huenda ikafungwa Shule nyingine tena kwa tatizo la choo.




                   Hii ni moja ya picha ya choo ya shule hiyo
Shule ya Msingi Kilimani iliyopo kata ya Nyasura Halmashauri ya Mji wa  Bunda mkoani Mara huenda ikafungwa kufuatia Kamati ya shule hiyo kumuandikia mhutasari Mkurungezi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda Janeth Mayanja wakiomba kufungiwa shule yao kwani choo ya shule hiyo imejaa choo na kupelekea  wanafunzi shule hiyo kujisaidia nje ya jengo la choo na kwenye mashamba ambayo yapo karibu na eneo la shule hiyo.


Akizungumza na Radio Mazingira fm mapema leo Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Kyinza Juma amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya katika shule hiyo hivyo wameona kunyamaza  kimya sio suluhu ya jambo hilo.

Juma amesema asaivi ni musimu wa mvua hivyo wasipochukuwa hatua za haraka asaivi inaweza kuleta madhara makubwa kwa wanafunzi hao kwani choo hicho kimejaa  na kwamba inafikia hatua hadi funza wanaonekana juu katika matundu ya choo hicho.

Aidha Juma amesema siku ya leo Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili amefika katika shule hiyo na kujionea hali ilivyo huku akisema hakuwa na taarifa kuhusiana na changamoto hiyo hivyo amepata taarifa kupitia Radio mazingira fm ndio akaamua kufatilia suala hilo.

Hata hivyo baada ya Mkuu wa wilaya ya Bunda mwl.Lydia Bupilipili kupata taarifa hizi kupitia kituo hiki ameamua kufuatilia suala hilo na kusema kuwa ni kweli amejionea hali hiyo na kwamba tayari ameshazungumza na Mkurungezi wa Halmashauri ya mji wa Bunda na hatua zimeanza kuchukuliwa.

No comments:

Post a Comment