MABINGWA
watetezi, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara baada ya kuibamiza Stand United mabao 3-1 katika mchezo
uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo
unaifanya ya kocha George Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel
Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali kufikisha pointi 46
baada ya kucheza mechi 21.
Yanga sasa
wanalingana kwa pointi na vinara wa muda mrefu msimu huu, Simba SC ingawa
mabingwa hao watetezi wamecheza mechi moja zaidi.
Katika
mchezo wa leo, mabao ya Yanga SC yamefungwa na beki wa Stand United, Ally Ally
aliyejifunga, kiungo Ibrahim Ajib na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa.
No comments:
Post a Comment