Nyumbani kumenoga Maxmillan madoro arejea CCM. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday, 9 March 2018

Nyumbani kumenoga Maxmillan madoro arejea CCM.



Aliyekuwa diwani wa kata ya nyamuswa 2005-2015, na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la bunda kupitia chama cha dp 2015  maxmillian madoro amekihama chama chake na  kujiunga na ccm leo baada ya ujio wa makam mwenyekiti wa ccm taifa bara philipo mangula mjini bunda.

Bwana madoro amesema kuwa awali alikuwa ccm lakini aliamua kuondoka ndani ya chama hicho baada ya kutotendewa haki na kuwepo kwa rushwa za waziwazi katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Amedai kuwa amerejea ndini ya chama ccm baada ya kuona utendaji kazi mzuri wa serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na kurejea katika chama hicho lakini pia ameambatana na baadhi ya wanachama watatu kujiunga ccm kutoka DP na kueleza kuwa wapo wanachama wengi wanaoitaji kujiunga na ccm lakini wameshindwa kufika mjini kutoka nyamuswa na kuamua kumkabidhi madoro kadi zao ili azikabidhi kwa makam mwenyekiti wa ccm taifa bara bwana philipo japhet mangula.

No comments:

Post a Comment