Msanii wa
nyimbo za asili kutoka Nyanda za juu
kusini Songwe mwenye masikani yake Jijini
Daressalaam anayefahamika kama
Tulivundwe Mwawalo ameachia wimbo
mpya unaowataka wadada pamoja na
wamama kulea watoto.
Tulivundwe
amesema hayo wakati akiutamburisha wimbo
wake mpya kwa wapenzi na wakazi wa kanda ya ziwa unaokwenda kwa jina la Sungaga umwana yaani tulee
watoto uliosikika kupitia kipindi cha kwetu kwanza ya 91.7 mazingira fm ambapo aliuachia kwa
mara ya kwanza.
Akizungumzia wimbo
huo ulioandaliwa katika studio za
Tivol zilizopo Jijini Mwanza Tulivundwe
amesema kuwa ametumia lugha ya kinyiha,Kiswahili
pia ameweka vionjo vya kisukuma katika wimbo huo ambapo amewaomba mashabiki wake waupokee kwa mikono miwili.
Kwanza kabisa napenda kuwashukuru
wenyeji wangu na wadau wote wa Bunda aah! kitu ambacho naweza kusema kwamba nimewaletea
nyimbo mpya inaitwa Sungaga umwana
naombeni muipokee kwa moyo na kwa upendo nawapenda sana na ndomaana nimeamua
kuwafateni hadi huku Bunda.alisema Tulivundwe.
Tulivundwe
ameachia wimbo huo uliobeba ujumbe mzito
kwa wale wenye tabia ya kutoa mimba pamoja na kutupa watoto wao wa kuwazaa
ikiwa ni siku chache tu kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia ambayo ufanyika march
nane kwa kila mwaka.
Pia
tulivundwe amewahi kutamba na vibao kama rafiki gani,tuilinde ngozi yetu,kasuku
aliyomshirikisha Cos B sasa amekuja na Sungaga umwana ambapo amesema maandalizi
ya video tayari yanaendelea.
Akizungumzia
soko la muziki wa asili lilivyo kwa sasa tulivundwe amesema vyombo
vya habari nchini bado vimeegemea kusuport muziki wa bongo fleva na
kuwasahau wasanii wanaofanya muziki wa asili.
Kitu ambacho nachojua kwa upande
wangu mimi ni support kwa upande wa media upande wa radio wametusahau tunaofanya
traditional wameegemea upande wa bongo fleva wamesahau muziki wa kwao ambao ni
utamaduni wao lakini sisi wa muziki wa asili hatujapewa chance hatuna vipindi
ambavyo vinapiga muziki wetu kwa mfano labda jumatano .alisema
Tulivundwe.
Hata hivyo
tulivundwe ameviomba vituo vya radio na tv nchini kutoa ushirikiano kwa kusuport kazi za wasanii wa muziki wa asili ili kufanya
wasanii wa muziki huo kujulikana kitaifa na kimataifa akitolea mfano wa waimbaji wa makhirikhiri ambao
wamevuka boda kutokana na support kutoka kwao.
No comments:
Post a Comment