Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mara, Jafary Mohammed amesema kuwa tayari jeshi la polisi
linawashikiria watu wanne kufuatia tukio la kifo cha aliyekuwa mmiliki wa wa mabasi ya Super Sami, Samson
Josiah.
Mwili wa
Samson Josiah umekukutwa
mto Ndabaka eneo la Bunda –Lamadi ukiwa umewekwa kwenye mifuko.
Radio
Mazingira fm imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafary Mohammed kwanjia
ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo ambapo amesema hadi sasa
wanawashikiria watu wane na kwamba bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa
tukio hilo.
Aidha Jafary
amesema chanzo cha kifo cha mmiliki wa mabasi hayo bado hakijajulikana lakini
upelelezi unaendelea ili kubaini nini kisa hasa cha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment