Picha
ya muonekano wa soko hilo
Wafanyabiashara ndogondogo
katika genge la Nyasura kata ya Nyasura Halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa
Mara wamesema kama serikali ya Halmashauri
ya mji wa Bunda inataka iwahamishie katika soko la manjembe basi ni vizuri hata
mnada na stand ya magari ikaanzishwa huko ili kuleta chachu ya biashara katika
eneo hilo.
Wafanyabiashara hao Wametoa ombi hilo leo wakati wakizungumza na
mazingira fm katika genge la Nyasura ambapo wamesema kuwa wao hawajakataa na
hawapingani na serikali kuhusu kuhama bali serikali iwaboreshee mazingira ya
soko ili waweze kuifanya bishara vizuri.
Wamesema tayari
wameshapewa samas ya kuhama hapo hivyo nao wanasubiri kupewa mrejesho wa nini
serikali inafanya juu ya uboreshaji wa soko hilo.
Kwa upande wa
mwenyekiti wa genge hilo la Nyasura Petro Chakoma amesema ameshafika katika
soko hilo la manjembe na kujionea hali halisi ilivyo ambapo hali bado ni mbaya
katika muonekano wa soko hilo ikiwa ni pamoja na mazingira ya soko kuwa machafu
ndani na nje ya soko.
Hatua ya kuhamishwa kwa wafanyabiashara inajiri
baada ya Diwani wa Kata hiyo Mwamba Mangambo Wasira kusika kupitia radio
mazingira fm akisema kuwa ni moja ya ahadi yake kipindi anaomba kura kwa
wananchi na kwamba uhamishaji huo si wale tu wanaofanyia biashara zao katika
genge la nyasura bali ni kwa wote ambao wanafanyabiasha katika mazingira
hatarishi kama vile kandokando ya barabara na maeneo kama hayo ndani ya
Halmashauri ya mji wa mji wa Bunda.
No comments:
Post a Comment