Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Miyombo (32), mkazi wa Kata ya
Hombolo, Bwawani mkoani Dodoma amenusurika kufa baada ya kukatwa
koromeo na mumewe wake akiyejulikana kwa jina la Mgowela Anderson.
Chanzo
cha kisa hicho kilichotokea Mei 16, mwaka huu kinaelezwa ni wivu wa
kimapenzi ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikutwa na mwanamume mwingine
ndipo mumewe akamjeruhi kwa kumkata na panga kwenye koromeo na kukimbia.
Akizungumza
kwa tabu huku akilia, Mary ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma amesema siku ya tukio akiwa ametoka kuuza
pombe kilabuni kijijini hapo alifika nyumbani kwake na kwenda anapoweka
fedha zake ambapo aligundua 1,000 haipo jambo lililosababisha kumuuliza
mume wake huyo.
“Nilipomuuliza
tu kama amechukua hiyo hela ndipo kipigo kilipoanza hadi kufikia hatua
ya kunikata na panga shingoni, yaani simtaki tena yule mwanamume kwani
hii ni mara ya tatu ananipiga na kunijeruhi na nimekuwa nikimsamehe
lakini kwa hili simtaki tena,” amesema Mary.
Mganga
Mfawidhi wa hiyo, Caroline Damian amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo
hospitalini ambaye alilazwa wodi namba 10 na tayari amesharuhusiwa.
Hata hivyo, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.
No comments:
Post a Comment