Hali mbaya ya miundombinu iliyopo katika kituo cha
afya cha Natta kilichopo wilayani Serengeti mkoani Mara kimewaingiza matatani
baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo mkurugenzi,Diwani,Mwenyekiti wakijiji
pamoja na Daktari kwakushindwa kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wanaofika
kituoni hapo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoawa Mara Adamu Malima
wakati wa Ziara yake wilayani Serengeti alipofika kukagua mradi wa ujenzi unaoendelea
katika kituo cha afya cha Natta ndipo kulipobainika changamoto mbalimbali zinazokikabili
kituo hicho.
Katika hali isiyodhaniwa kituo hicho hakinaumeme katika
baadhi ya maeneo ikiwemo wodi la wazazi jambo ambalo limewalazimu wanawake wanaoenda
kujifungua kutumia tochi katika huduma zao zamsingi na hata kwa maeneo muhimu kamachooni
pia hakuna umeme.
Dina Joseph mkazi wa kijiji cha Natta amemueleza mkuu
wa mkoa kwamba kwa sikumbili sasa tangu afike kituoni hapo hakuna umeme wanalazimika
kutumia mwanga wa tochi lakini kwa wale ambao hawana tochi wanatembea gizani jambo
ambalo nihatarishi kwamaisha yao.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mara amesikitishwa na kitendo
hicho na kuwaagiza viongozi wanaosimamia kuchukua hatua za haraka kutatua matatizo
hayo pasipo kujali itikadi za vyama vyao.
No comments:
Post a Comment