WACHUNGAJI watatu wamenusurika kipigo kutoka kwa
wananchi, baada ya kushindwa kumfufua marehemu katika Kijiji cha Sitalike
Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Wachungaji hao walifika kijijini hapo wakidai kuwa wanao uwezo wa kumfufua
marehemu mwanakijiji mwenzao aliyefariki dunia hivi karibuni na kuzikwa kwenye
makaburi ya Kijiji hicho.
Akisimulia tukio hilo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Christopher Angelo, amesema
kuwa tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi limetokea Mei 7 kijijini hapo.
Amesema kuwa wachungaji hao ambao walikuwa watatu walifika kwenye ofisi ya
Kijiji na kujitambulisha kuwa wao ni wachungaji wanatoka katika Kijiji cha
Nsimbo na watakuwapo kijijini hapo wakiwa wameitwa na ndugu wa marehemu, Raymond
Mirambo aliyefariki dunia siku moja na kuzikwa kijijini hapo.
Mwenyekiti huyo alisema kutokana na kujitambulisha kwa wachungaji hao kwenye
ofisi ya kijiji, uongozi wa kijiji uliwaruhusu wachungaji hao kufanya maombi
hayo ya kumfufua marehemu huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment