Wanafunzi wawili wamekufa maji baada ya
kivuko walichokuwa wakitumia kuzama katika eneo la Chulwi wilayani
Mkuranga mkoani Pwani, huku watu wazima 10 wakiokolewa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Ali
Hengo aliye eneo la tukio amesema wanafunzi hao walikuwa wakivuka kwenye
kivuko ambacho sio rasmi wanachokitumia kila siku kwa ajili ya kwenda
shuleni huku wakiwa na wananchi wengine, ambacho ndiyo kimezama na
kusababisha vifo hivyo.
"Kuna watu walikuwa wakivuka pamoja na
wanafunzi sasa wakazama, baada ya kuzama watu wazima waliokolewa lakini
wanafunzi wawili, mmoja amekutwa amekufa mwingine amezama kwenye maji na
hajulikani alipo, amesema Ali Hengo.
Ali ameendelea kuelezea hali halisi ya
eneo hilo na kusema kwamba ..."Hiyo sehemu kuna kivuko watu wanavuka
kienyeji sasa wanatumia mipira ya matairi ya gari ama miti kutengeneza
tengeneza kama vingalawa tu vidogo vya kuvuka, sasa kutokana na mvua
iliyonyesha ndio zikasababisha madhara haya".
No comments:
Post a Comment