Zahanati ya
kijiji cha kurusanga iliyopo kata
ya Salama wilaya ya Bunda Mkoani Mara
imepokea msaada wa Darubini kutoka kwa Diwani wa Kata ya
Ketare mh.Mramba Simba Nyamkinda
itakayotumika kupima magonjwa
mbalimbali na kuboresha huduma katika zahanati
hiyo.
Darubini
hiyo yenye thamani ya shiliingi milioni
moja inayotumia nishati ya umeme na jua imetolewa jana jumamosi na mh.Mramba Simba
Nyamkinda ambae ni diwani wa kata
ya Ketare baada ya kuona ukosefu wa kifaa hicho katika zahanati hiyo.
Akizungumza wakati
wa kupokea kifaa hicho Daktari msimamizi wa Zahanati hiyo Sajadi
Hassani amemshukuru mheshimiwa Mramba
ambapo amesema awali walikuwa wakitoa huduma kwa kukisia ugonjwa lakini sasa darubini hiyo itawasaidia kubaini
magojwa na kutoa huduma kwa uhakika.
Pia Mramba
amemtaka daktari wa kituo hicho kutunza vizuri kifaa hicho ili kiwasaidie wananchi kupata huduma za vipimo ambapo amewaomba wasikipoteze kama walivyo poteza Darubini
aliyoitoa hapo awali.
Wakati huo
huo mh.Mramba ametoa pawa miksa katika kanisa la EAGT la kurusanga na kuahidi kutoa mifuko kumi ya
sementi ili kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment