RC MARA, MEJA JENERALI SULEIMANI MZEE
Imeelezwa kua katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani
Mara Wilaya ya Bunda inaongoza kwa wizi
wa vifaa vya ujenzi wa miradi hiyo jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za
serikali.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoa wa Mara Meja jenerali Sulemani Mzee katika ziara ya
kukagua mradi wa ujenzi wa chujio la maji Nyabehu wenye gharama ya zaidi ya Tsh. bilioni 10 na ambao utanufaisha wakazi wote wa
wilaya Bunda pindi utakapo kamilika.
Akiwa katika eneo la mradi huo RC Mzee amesema suala la wizi katika
miradi ya serikali linasikitisha hasa wilaya ya Bunda na kuwataka wananchi kuwa
walinzi wa miradi hiyo.
Hata hivyo mkuu wa mkoa amewapongeza
BUWSSA kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika kutekeleza mradi
huo huku akiwata wasimamizi kurekebisha sehemu zenye kasoro ili kuendana na
thamani ya pesa inayotolewa naserikali.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Dr. Vicent Naano amemshukuru mh.
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha
ujenzi wa chujio hilo huku akiwataka BUWSSA kuweka mfumo wa kisasa wa ulinzi
utakao saidia kudhibiti uharibifu wa mradi huo.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kaimu mkurugenzi wa
mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira Bunda BUWSSA Ester Gilyoma amesema utekelzaji wa mradi huo umefikia
asilimia 99 na sasa wananchi wanapata maji safi na salama tofauti na ilivyo kua
awali.
No comments:
Post a Comment