Wananchi wa mtaa wa Tamau kata ya Nyatwali wakiwa katika mkutano kujadili hatima yao katika eneo hilo. |
Wananchi wa Mtaa wa Tamau kata ya Nyatwali Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wameuomba uongozi wa Wilaya hiyo kufanya mikutano ya mara kwa mara katika maeneo yao ili kuwawezesha kupata taarifa na ufafanuzi wa baadhi ya mambo yanayohusu mchakato wa kuhamishwa katika eneo hilo.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa mtaa huo eneo la shule ya msingi Tamau jana tarehe 21 April 2023 wenye lengo la kuelimisha wananchi kufungua akaunti za benki na kuwapa taarifa juu ya utaratibu uliotolewa kwa wale wenye malalamiko mbalimbali, wananchi hao wamesema ni vema uongozi wa Wilaya ukawa na utaratibu wa kufika ili kuwasikiliza kama ilivyokuwa sehemu ya ahadi zao.
Mkaazi wa Tamau akichangia mawazo yake katika mkutano wa wananchi na viongozi wa mtaa huo. |
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Asafu Ernest Owiti amesema mtathimini mkuu wa taifa ameunda kamati inayoongozwa na Diwani wa kata hiyo huku katibu wake akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda ili kufuatilia malalamiko mbalimbali ya wananchi kisha kutoa mapendekezo ambayo yatawasilishwa kwa mtathimini kwa hatua zaidi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Tamau, Asafu Ernest Owiti
Dotto Kihiri Mirumbe, Afisa Mtendaji Mtaa wa Tamau akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja kwa wananchi wa Tamau.
No comments:
Post a Comment