Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa za kifo cha mwanasiasa na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe kilichotokea leo.
Rais ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40 Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbinge na Waziri aliyetumikia nchi yetu kwa weledi.
Pole kwa familia, ndugu, jamaa&marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina.
No comments:
Post a Comment