Uwepo wa Sheria Mahususi inayopinga vitendo vya Ukeketaji Nchini Tanzania itasaidia kutokomoza Ukatili huu kwenye Jamii zilizoathirika na huo utamaduni3
Hayo yamesemwa na wadau wa kupinga Ukeketaji Nchini Tanzania katika mafunzo kwa waandishi wa habari ambapo lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kuhakikisha Ukeketaji unaisha Nchini Tanzania
Akizungumza katika kikao hicho mkaguzi msaidizi wa Polisi Cloud Mtweve ambaye ni mratibu wa mradi wa kupinga Ukeketaji unaovuka Mipaka amesema Tanzania hatuna Sheria Mahususi inayopinga vitendo vya Ukeketaji japokuwa tunavyo vifungu Vya Sheria vinavyopinga masuala ya Ukatili wa kijinsia akitolea mfano Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 kifungu na 169 A kifungu kidogo Cha (1) na (2) malejeo ya mwaka 2022, pia Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, kwa pamoja zinakataza kumfanyia mtoto huo Ukatili.
Aidha Mtweve ameeleza kuwa changamoto inayowakumba ni suala la ushahidi ambapo amesema kwa upande wao kama jeshi la polisi Ili kesi iweze kusikilizwa mahakani na kutolewa hukumu ni lazima awepo mlalamikaji na shahidi pili Ili mahakama iweze kutoa hukumu inatakiwa ijiridhishe pasipo kuacha shaka.
Amesema mara nyingi kesi za ukeketaji zinashindwa kufika mwisho kutokana na ugumu wa kupata walalamikaji pia mashahidi hivyo ingekuwepo Sheria ya kuwabana hata wazee wa kimila, mangariba, wazazi na walezi, wanaohusika wote kwenye sherehe hizo, marufuku ya ahadi ya zawadi ingeweza kusaidia.
Kupitia kwa Michael Marwa Mkuu wa Miradi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la C – SEMA kwa kishirikina na UNFPA ambao ndiyo wadhamini wa mafunzo haya amesema mafunzo haya yamewalenga waandishi wa habari kwa lengo la kwenda kuhihamasisha Jamii na kuishawishi mamlaka ili Kwa juhudi za pamoja suala la Ukeketaji hasa unaovuka mipaka (Cross Border FGM) unakwisha ifikapo 2030 kwa Mujibu wa mkakati uliyowekwa na mataifa matano ukanda wa Afrika ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment