Watoto wa Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana KKKT Bunda wakiwa katika studio za Radio Mazingira Fm |
Watoto kutoka kituo cha Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana kanisa la KKKT Bunda leo 10 June 2023 wametembelea kituo cha Radio Mazingira Fm ili kujionea uendeshaji, maandalizi, urushaji wa vipindi pamoja na kushiriki katika kipindi cha Watoto.
Debora Patrick, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda. |
Wakizungumza baada ya kufika na kujionea shughuli mbalimbali katika kituo cha Radio Mazingira Fm, wamepongeza namna inavyoendesha shughuli zake na kuandaa vipindi vinavyogusa jamii.
"Tumejifunza vitu vingi sana hapa na nina furaha kubwa sana. Wito wangu kwa jamii tuendelee kuisikiliza Radio Mazingira kwasababu ni radio inayotoa taarifa za ukweli na ni radio ambayo ipo karibu na jamii yetu" Debora Patrick
Makaranga Maduhu, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda. |
No comments:
Post a Comment