Vijana FPCT Neno la Neema bunda, waadhimisha wiki ya vijana kwa kutembelea wodi ya wazazi kituo cha afya Bunda. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday, 21 June 2023

Vijana FPCT Neno la Neema bunda, waadhimisha wiki ya vijana kwa kutembelea wodi ya wazazi kituo cha afya Bunda.

 

Umoja wa vijana kanisa la FPCT Neno la neema chini ya mchungaji Omoso wametembele wodi ya wazazi kituo cha afya bunda ikiwa ni sehemu ya sherehe za wiki ya vijana kanisani hapo

Akizungumza na radio mazingira fm mwenyekiti wa vijana wa kanisa hilo Bade Winford amesema katika wiki hiyo ya vijana wamefanya mambo mengi ikiwemo kueneza habari njema za injili kwa vijana, michezo , pamoja na tukio la leo la kutembelea wodi ya wazazi kituo cha afya cha bunda ambapo wanatambua mchango wao wa kuendeleza uumbaji wa mungu.

Bade Winford

Aidha amesema wiki hiyo ya vijana ilianza tangu tarehe 12 mwezi  June na inatarajia kutamatika hapo kesho june 18 Kwa ibada itakayoongozwa na vijana.

Kwa upande wao akina mama waliojifungua kituo cha afya wameshukuru vijana wa  FPCT  Neno la Neema kuja kuwatembelea pia zawadi walizowaletea kwa maana ni mara chache sana kwa vijana kuwa na moyo kama huo pia wamewashukuru madaktari na wauguzi wanaowahudumia maana wanapata huduma nzuri pindi wanapofika kujifungua.


No comments:

Post a Comment