Mtandao wa radio za kijamii Tanzania TADIO waendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka redio za kijamii namna ya kutumia mitandao ili iwe fulsa kwao,
Na Catherine Msafiri na Avelina Sulusi
Wito umetolewa kwa viongozi wa redio za kijamii kusimamia waandishi ili mafunzo ya matumizi ya redio mtandao wanayoyapata yasaidie kuleta mabadiriko katika redio zao
Wito huo umetolewa Julay 7,2023 na Hilali Alexerder Luhundwa ambaye ni muhariri wa Radiotadio iliyoko chini ya Mtandao wa radio za kijamii Tanzania TADIO wakati akizungumza na Mazingira Fm alipofika kituoni hapo kwaajiri ya kutoa mafunzo ya namna ya kuchapisha habari katika mtandao.
lengo kuu likiwa ni kuziunganisha redio za kijamii zitumie jukwaa hilo kubadirishana habari.
Hilali amebainisha kuwa kutokana na mafunzo wanayotoa wanatarajia kuona radio zinabadirika na kuwa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia waandishi wanatumia mwanya huo kama fulsa kwao hasa ukizingati teknolojia inabadirika kila siku hivyo waandishi na redio zinalazimika kubadirika kulingana na teknolojia.
Aidha amebainisha kuwa TADIO kama Mtandao wa radio za kijamii Tanzania wamelazimika kuanzisha jukwaa la redio mtandao lengo kuu likiwa ni kuziunganisha redio za kijamii zitumie jukwaa hilo kubadirishana habari.
Kwa upande wao waandishi wa habari wa kituo cha radio Mazingira Fm wameishukuru tadio kwa mafunzo waliyoyapata na kutokana na mafunzo hayo wamejua namna ya kuchapisha habari kwenye mtandao pia kutumia mitandao ya kijamii kama fulsa .
Aidha wameiomba TADIO kuendelea kutoa mafunzo haya ili yaendelee kuwajenga na kuendana na kasi ya mabadiriko ya technolojia duniani
No comments:
Post a Comment