Ili kuhakikisha vijana wanaendelea kujikwamua kimaisha wametakiwa kuchanagmkia fursa zinazotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo ya asilimia kumi kutoka halmashauri.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa vijana mkoani Mara kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ili kujikwamua kimaisha na kuondokana na utegemezi.
Wito huo umetolewa leo na Mbunge viti maalumu kupitia kundi la vijana Mhe Juliana Didas Masaburi katika baraza la Umoja wa vijana chama cha mapinduzi CCM lililofanyika ukumbi wa Helieth Bunda mjini
Mhe Masaburi amesema badala ya vijana kuangaika kutafuta viongozi kwenye simu ili kupata fursa za ajira au kazi zinanotolewa, wanatakiwa kuziomba fursa hizo kwa wingi ili wachaguliwe
Aidha katika kuwasaidia vijana kuwa na miradi itakayowasaidia kuendesha jumuiya yoa Mhe Juliana amehaidi kuto mashine moja ya kufyatua tofari kwa vijana wa CCM wilaya ya Bunda.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavia Chacha Nyamigeko akiwa mgeni mualikwa katika baraza hilo amesema jumuiya ya umoja wa vijana ina changamoto ya ukosefu wa mradi wa kujiendesha ambpo amesema ili kuondokana na chanagamoto hiyo ameahidi pia kutoa mashine moja ya kufyatua tofari kwa jumuiya hiyo.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo mwenyekiti wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Mohamed Msafiri amesema kulingana na ukosefu wa chanzo cha mapata katika jumuiya hiyo kinapelekea hata maudhurio katika mabaraza kuwa kidogo
No comments:
Post a Comment