Mbio za mwenge kitaifa mwaka 2023 katika halmashauri ya wilaya Bnda imetembelewa miradi 7 ambapo miongoni mwa shughuli zilizofanyika ni uteketezaji wa zana haramu za uvuvi ikiwa ni jitihada za kulinda na kutunza mazingira.
Na Thomas Masalu
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 ameteketeza zana haramu za uvuvi zilizokamatwa hivi karibu na maafisa wa uvuvi wa Halmashauri hiyo katika mwalo wa Kibara Kata ya Kibara halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Akiteketeza zana hizo, Abdalah Shaibu Kaim amesema serikali haiwezi kufumbia macho uvuvi haramu hivyo ni vyema wananchi wakaachana na shughuli ya uvuvi haramu maana hailipi.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kuwa mabalozi wema katika utuzanji wa rasiliamali ili kizazi kijacho kifaidike na rasiliamali zilizopo.
Uteketezaji huo umefanyika leo katika eneo la mwalo wa Kibara ambapo pia choo cha matundu matano chenye lengo la uboreshaji wa mazingira kimezinduliwa.
Hiyo ikiwa ni miongoni mwa miradi kati ya miradi 7 iliyotembelewa na mwenge wa uhuru 2023 ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bunda.
No comments:
Post a Comment