Nyatwali: miti yakatwa, Nyaraka za tathimini ya fidia kuchukuliwa mikopo kisa ugumu wa maisha - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday, 14 July 2023

Nyatwali: miti yakatwa, Nyaraka za tathimini ya fidia kuchukuliwa mikopo kisa ugumu wa maisha

Baadhi ya miti iliyokatwa na wananchi wa Nyatwali kwa lengo la kuchoma mkaa ili wajikimu kimaisha, Picha na Edward Lucas

Zoezi la kuwaamisha wakazi wa kata ya nyatwali likiwa linaendelea katika hatua ya tathimini baadhi yao wanalia na hali ngumu ya maisha na njaa kutokana na kupigwa marufuku kufanya shughuri za uzalishaji na kulima mazao ya muda mrefu hali inayowapelekea kukata miti na kuingia kwenye mikopo umiza,

Na Edward Lucas

Ikiwa serikali bado inaendelea na mchakato wa kuwahamisha wakaazi wa  kata ya Nyatwali Halmashauri ya Mji wa Bunda, mapya yaibuka kwa wananchi kuanza kukata miti kwa ajili ya kuuza na kuchoma mkaa na kujitumbukiza kwenye mikopo kwa dhamana za nyaraka za fidia na tathimini ili kujikimu kimaisha.

Hayo yamebainika leo tarehe 13 July 2023 kupitia mahojiano ya Mazingira Fm na wananchi wa maeneo hayo mtaa wa Kariakoo wakati ilipowatembelea kwa lengo la kujua nini zaidi kinachoendelea katika zoezi la kuhamishwa.

Baadhi ya miti iliyokatwa na wananchi wa Nyatwali kwa lengo la kuchoma mkaa ili wajikimu kimaisha, Picha na Edward Lucas

Wamesema tangu ulipoanza mchakato wa kuhamishwa walielekezwa kutoendeleza makazi wala kutolima mazao ya muda mrefu jambo ambalo limepelekea baadhi kukosa uhakika wa chakula na makazi bora hivyo kujikuta wanaingia katika mikopo-umiza kwa kuweka dhamana nyaraka zao za fidia kwamba watarejesha baada ya kuwa wamelipwa fidia.

Hali hiyo imethibitishwa na Diwani wa Kata hiyo, Malongo Mashimo alipotafutwa na Mazingira Fm kwa njia ya simu na kusema kuwa kufuatia hali hiyo ameomba serikali iwasaidie wananchi kupata huduma ya mahindi ya bei nafuu na iharakishe mchakato kwani wameshindwa kujishughulisha na uzalishaji mali na shughuli zingine za maendeleo.

Malongo Mashimo Diwani wa Kata ya Nyatwali

Aidha katika hatua nyingine baadhi ya wananchi waliotathiminiwa maeneo yao yalioingia ndani ya maji maarufu kama ‘masanga’ wameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao huku wale waliokosa nafasi hiyo kwa kigezo cha kukosa hati za maeneo yao wakiiomba serikali iangalie namna ya kuwasaidia kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizokwamisha kupata hati hizo.

Mkazi wa kata ya Nyatwali

No comments:

Post a Comment