Watumishi wanne wa idara ya afya pamoja na dereva wao wamenusurika kifo baada ya gari lao kuwaka moto wakati wanatoka kutoa huduma ya uzazi wa mpango mtaa wa Kinyambwiga kata ya Guta Halmashauri ya Bunda Mjini
Na Adelinus Banenwa
Watumishi wanne wa idara ya afya kutoka Musoma na Bunda pamoja na dereva wao wamenusurika kifo baada ya gari lao kuwaka moto katika eneo la Manyamanyama Bunda barabara ya Mwanza Musoma.
Tukio hilo limetokea leo 21 july 2023 majira ya mchana ambapo watumishi hao walikuwa wakitoka hospital ya Manyamanyama kwenda Bunda mjini.
Akizungumza na mazingira fm Paul Christopher dereva wa gari hilo amesema wakati wanatoka hospitali ya manyamanyama aliona moshi ukitoka kwenye dashboard ndipo aliposimamisha gari ili kujua nini tatizo.
Christopher ameongeza kuwa baada ya kuona moshi umezidi walijitahidi kutumia kifaa cha kuzimia moto yaani fire extinguisher pamoja na mchanga lakini hawakufanikiwa kuuzima moto.
Kwa upande wake Dkt Lucy kiongozi wa msafara huo ameiambia mazingira fm kuwa moshi ndiyo umeanza kuonekana kwenye gari na harufu ya kitu kuungua ndipo alipomwambia dereva asimamishe gari na kushuka kisha kufungua bonet ya gari na kugundua tayarii moto umeshaanza kuwaka.
Aidha Dkt lucy amesema wanashukuru wametoka salama na vifaa vyao isipokuwa dereva ndo nyaraka zake zimeungua pia amewashukuru wananchi waliojitokeza kutoa msaada lakini gari lote limeteketea.
Watumishi hao walikuwa wanatoka kata ya Guta mtaa wa Kinyambwiga katika huduma ya uzazi wa mpango .
No comments:
Post a Comment