Madiwani Bunda DC wakubali kupitisha bajeti ya Tsh, 36,5 bilion
20 February 2025,

Baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limepitisha makadilio ya bajeti ya shilingi Bilion 36.5 kwa mwaka wa fedha 2025 na 2026
Na Adelinus Banenwa
Baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limepitisha makadilio ya bajeti ya shilingi Bilion 36.5 kwa mwaka wa fedha 2025 na 2026 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara ya watumishi, kulipa madeni, pamoja na matumizi mengine.
Bajeti hiyo imepitishwa leo tarehe 20 Feb 2025 katika baraza hilo liliketi kujadili ambapo pamoja na mambo mengine baraza hilo lilipitia mapendekezo ya kamati mbalimbali za halmashauri.
Kikao hicho kimeongozwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo mhe Keremba Irobi.

Katika ushauri wao madiwani hao wameshauri mkurugenzi pamoja na wataalamu kuzingatia maoni ya kamati katka utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kupeleka huduma mahala ambapo hazipo kama katika sekta za Elimu na Afya.

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salumu Mtelela ameipongeza halmashauri hiyo kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ambapo amesema kwa mwaka wa fedha 2023 na 2024 halmashauri hiyo ilikusanya zaidi ya malengo.
Mtelela amewahimiza watumishi wa halmashauri hiyo wakiongozwa na mkurugenzi kuendelea kukusanya mapato pia kumaliza miradi ambayo inaendelea kutekelezwa katika halmashauri hiyo.

Wakati huo huo baraza hilo la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limepitisha mapendekezo ya Bajeti ya Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA ya shilingi bilion 7.6 ikijumuisha fedha za upanuzi wa barabara milioni 800 fedha za mfuko wa jimbo bilion 1 na Fedha za tozo ya mafuta bilion 2.
Akizungumza katika baraza hilo kaimu meneja TARURA Bunda Muhandisi Hamad Munisi amesema endapo fedha hizo zikipitishwa zinakwenda kutekeleza hatua mbalimbali ikiwemo ujenzi wa makarvati, ufunguaji wa barabara mpya, ujenzi wa barabara za lami na ujenzi wa mitaro.
No comments:
Post a Comment